Just another WordPress.com site

Tume ya Kukusanya Maoni (The Constitutional Commission) inayoongozwa na Jaji Wariyoba imeanza kuzunguka mikoani nchini kukusanya maoni. Kwa mujibu wa Jaji Waiyoba, tume itaanzia mikoa ya Pwani, Manyara, Bukoba, Sinyanga, Kusini Unguja na baadaye mikoa mingine.

Waislamu wote mnaombwa kujiandaa kutoa maoni yenu kwenye tume hiyo na njia za kutoa maoni ni tatu kama ifuatavyo;-

1. Kuongea au kuwasilisha maoni yetu kwa mdomo katika mikutano ya mabaraza ya maoni ya katiba itakayoitishwa na Tume ya Katiba.

2. Kuomba kuonana ana kwa ana na Tume ya Katiba na kutoa maoni yetu. Waislamu mnaweza kutuma ombi la kuonana na tume hiyo watakapokuijieni katika maeneo yenu.

3. Kuwasilisha maoni kwa maandishi.

Zingatieni kutoa maoni yetu ya kitaifa ingawa hamkatazwi kuongeza maoni yenu mtakayoona yanafaa kwa maslahi ya Uislamu na Waislamu.

 

Mwenyekiti

Jukwaa la Waislamu la Kuratibu Mabadiliko ya Katiba Tanzania (JUWAKATA)

Comments on: "TUME YA KATIBA YAANZA KUKUSANYA MAONI" (2)

  1. OMARY JAILANI said:

    INSHAALLAH SHEKH WANGU THANX 4 INFORM US JAZAKUMULLAHU KHAYRA

Leave a reply to OMARY JAILANI Cancel reply