Just another WordPress.com site

Archive for September, 2012

Kanisa Lajipanga Kutoa Maoni ya Katiba Mpya

Assalaam alaykum.

 

Awamu ya kwanza ya utoaji maoni kwa tume ya katiba ilimalizika mwezi Julai tarehe 30 na awamu ya pili kuanza Agosti Mosi kwa mikoa mingine minane safari hii Tanzania Bara pekee.

Taarifa kutoka sehemu mbali mbali ambazo tume inapita zinaonesha kwamba wakristo safari hii wamejipanga vizuri kutoa maoni yao na mambo makubwa wanayoyapinga ni Mahakama ya Kadhi, Uvaaji wa Hijabu mashuleni na vyuoni na Tanzania kujiunga na OIC.

Jukwaa la Kuratibu Maoni ya Waislamu katika Katiba mpya Tanzania (Juwakata) linawahimiza waislamu wote kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yetu kama yalivyowafikia kupitia kijitabu chetu na muwahimize na wengine kufika katika mabaraza ya kutoa maoni.

Pia mnaweza kuandika maoni yenu na kuyakabidhi kwa wajumbe wa tume hiyo watakapowafikia katika maeneo yenu. Mnaweza pia kuchangia kwa mtandal kupitia http://www.katiba.go.tz.

Shime ‘alaykum tuinusuru dini yetu kwa kutokuruhusu maslahi ya Uislamu kuchezewa. Tukumbuke kuwa nchini Canada adhana imepigwa marufuku.

Mwenyekiti-Juwakata

 

 

Advertisements

Tag Cloud